Maradhi ya macho yaendelea kutatiza Wakaazi Mombasa
Zaidi ya watu elfu moja kaunti ya Mombasa wanaugua maradhi ya macho mekundu yaliyoripotiwa kuzuka katika kaunti hii.
Idara ya Afya kaunti ya Mombasa imethibitisa hilo huku ikibaini kuwa idadi hiyo huenda ikawa ni kubwa zaidi kutokana na baadhi kuwa hawajafika katika vituo vya afya.
Idara hio iliendelea kutoa tahadhari kwa wakaazi wote na hasa wazazi kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo.
Kulingana na Afisa wa Afya kaunti ya Mombasa Abdallah Deleno, watoto na watu wazima ni miongoni mwa waathiriwa.
Deleno aliwataka wakazi kutokuwa na hofu akiyataja maradhi hayo kuwa ya kawaida japo akitoa himiza ya kuchukua tahadhari ili kujilinda na maradhi hayo ikiwemo kudumisha usafi kwa kunawa mikono kwa maji na sabuni na kujizuia kushika macho kila mara.

Comments
Post a Comment