Ruto yu zuarani nchini Italia



Rais William Ruto ameondoka humu kuelekea  nchini  Italia ambako anatarajiwa kuhudhuria kongamano la Italia na Afrika.

Dhamira ya  kongamano hilo la ni kuboresha uhusiano kati ya Italia na bara Afrika.

Kongamano hilo linatarajiwa  kuweka wazi mpango makhsusi wa taifa la Italia unaolenga kubadili jinsi imekuwa ikihusiana na bara hili.

Nyanja mbali mbali za ushirikiano zitazungumziwa kwenye kongamano hilo kama vile kujitosheleza kwa chakula, utamaduni, elimu, elimu ya kiufundi, usalama wa kawi, uchumi na maendeleo ya miundomsingi.

Ushirikiano katika kukabiliana na ulanguzi wa binadamu na ugaidi vitajadiliwa pia kwenye kongamano hilo.

Rais Ruto katika wadhifa wake kama mwenyekiti wa kamati ya viongozi wa nchi za Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi atahutubia kongamano hilo.


Comments

Popular posts from this blog

Youths,drivers of economic change

Washukiwa wa mauaji Shakahola wakana Mashtaka