Siku ya Kimataifa ya Kawi Safi

                     


Kenya siku ya Ijumaa Januari 26, ilijiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nishati Safi. 


Kenya imejiunga na mataifa mengine kuadhimisha siku ya nishati safi ulimwenguni.                            Sherehe hizo huadhimishwa  tarehe 26 Januari kila mwaka kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni mfumo endelevu wa nishati safi katika siku za usoni yaani (“Clean Energy: The transition to a sustainable future”.)


Katika kaunti ya Mombasa maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi ya amani kutoka Bustani ya Uhuru, eneo la Mapembeni hadi eneo la Treasury Square ambako kilele cha maadhmisho hayo yalifanyika kwa maonyesho mbalimbali na hotuba za viongozi.


Waziri wa uchukuzi kaunti ya Mombasa Daniel Manyara alisema wizara yake inafanya mazungumzo kuhakikisha utumizi wa nishati safi kwenye sekta ya usafiri.

Comments

Popular posts from this blog

Youths,drivers of economic change

Washukiwa wa mauaji Shakahola wakana Mashtaka