Posts

Showing posts from January, 2024

Washukiwa wa mauaji Shakahola wakana Mashtaka

Image
 Jumla ya washukiwa 39 wa mauaji ya halaiki ya watu katika msitu wa Shakahola wamekana mashataka yote 17 dhidhi yao mbele ya Hakimu Nelly Chipchirchir katika mahakama ya watoto ya Tononoka hapa mjini Mombasa. Wakiongozwa na mhubiri tata Paul Mackenzie washukiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kuwatesa watoto kinyama, kusababisha vifo vya watoto kinyume cha sheria,kuwanyima haki yao ya elimu na chakula miongoni mwa mashtaka mengine. Mawakili wa washukiwa hao wakiongozwa na Wycliffe Makasembo waliiomba mahakama kupewa stakabadhi za zenye ripoti ya ushahidi wa madai dhidi ya wateja wao ili wazihakiki na kuzitathmini, ombi ambalo mahakama ya watoto ya Tononoka ilikubaliana nalo.

Ruto yu zuarani nchini Italia

Image
Rais William Ruto ameondoka humu kuelekea  nchini  Italia ambako anatarajiwa kuhudhuria kongamano la Italia na Afrika. Dhamira ya  kongamano hilo la ni kuboresha uhusiano kati ya Italia na bara Afrika. Kongamano hilo linatarajiwa  kuweka wazi mpango makhsusi wa taifa la Italia unaolenga kubadili jinsi imekuwa ikihusiana na bara hili. Nyanja mbali mbali za ushirikiano zitazungumziwa kwenye kongamano hilo kama vile kujitosheleza kwa chakula, utamaduni, elimu, elimu ya kiufundi, usalama wa kawi, uchumi na maendeleo ya miundomsingi. Ushirikiano katika kukabiliana na ulanguzi wa binadamu na ugaidi vitajadiliwa pia kwenye kongamano hilo. Rais Ruto katika wadhifa wake kama mwenyekiti wa kamati ya viongozi wa nchi za Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi atahutubia kongamano hilo.

Shule ya upili ya kaya tiwi yafungwa

Image
Shule ya upili ya Kaya Tiwi katika kaunti ya Kwale imefungwa kwa muda, baada ya wanafunzi kuzua rabsha katika shule hiyo mapema leo asubuhi, wakidaiwa kuzua vurugu hizo wakipinga uhamisho wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Chigamba Chilembi

Maradhi ya macho yaendelea kutatiza Wakaazi Mombasa

Image
  Zaidi ya watu elfu moja kaunti ya Mombasa wanaugua maradhi ya macho mekundu yaliyoripotiwa kuzuka katika kaunti hii. Idara ya Afya kaunti ya Mombasa imethibitisa hilo huku ikibaini kuwa idadi hiyo huenda ikawa ni kubwa zaidi kutokana na baadhi kuwa hawajafika katika vituo vya afya. Idara hio iliendelea kutoa tahadhari kwa wakaazi wote na hasa wazazi kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo. Kulingana na Afisa wa Afya kaunti ya Mombasa Abdallah Deleno, watoto na watu wazima ni miongoni mwa waathiriwa. Deleno aliwataka wakazi kutokuwa na hofu akiyataja maradhi hayo kuwa ya kawaida japo akitoa himiza ya kuchukua tahadhari ili kujilinda na maradhi hayo ikiwemo kudumisha usafi kwa kunawa mikono kwa maji na sabuni na kujizuia kushika macho kila mara.

Siku ya Kimataifa ya Kawi Safi

Image
                      Kenya siku ya Ijumaa Januari 26, ilijiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nishati Safi.  Kenya imejiunga na mataifa mengine kuadhimisha siku ya nishati safi ulimwenguni.                            Sherehe hizo huadhimishwa  tarehe 26 Januari kila mwaka kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni mfumo endelevu wa nishati safi katika siku za usoni yaani (“Clean Energy: The transition to a sustainable future”.) Katika kaunti ya Mombasa maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi ya amani kutoka Bustani ya Uhuru, eneo la Mapembeni hadi eneo la Treasury Square ambako kilele cha maadhmisho hayo yalifanyika kwa maonyesho mbalimbali na hotuba za viongozi. Waziri wa uchukuzi kaunti ya Mombasa Daniel Manyara alisema wizara yake inafanya mazungumzo kuhakikisha utumizi wa nishati safi kwenye sekta ya usafiri.

Youths,drivers of economic change

Image
  As a young person from Kenya , I know I play a crucial role in driving economic growth and social prosperity. I recognize that the creativity of the human person is the country’s greatest resource. To maximize this potential, an emphasis should be placed on providing youth with access to education and skills training. This equips us with proper tools to face the challenges that come our way and allows us to be globally competitive. Presently, some youth face difficulties accessing proper employment opportunities. Exposure to situations of abuse, discrimination, or exploitation is also a problem. Neglecting youth needs not only increases vulnerability, but also poses a threat to a country’s productivity. We cannot afford to waste the potential of the youth by not prioritizing their education and training. With proper employment opportunities in place, young people may excel in various fields. We should focus on the things that drive excellence and not on the points that limit us a...